GRAĂA MACHEL TRUST NA WASHIRIKI WA MARA ALLIANCE WAMEDHAMIRIA KUTEKELEZA MRADI MKUBWA KWA KUBAINI, KUWAANDIKISHA NA KUREJESHA WATOTO 20,000 WALIO NJE YA SHULE IFIKAPO DESEMBA 2017 KATIKA MKOA WA MARA, TANZANIA
Musoma, Tanzania, Aprili 5, 2016
Maelfu ya watoto kati ya miaka 7 na 14, mpaka sasa wameacha shule katika mkoa wa Mara, Tanzania, mradi huu shirikishi utakozinduliwa rasmi siku ya Jumanne umedhamiria kuwarudisha watoto hao mashuleni ndani ya miaka miwili.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Msaada wa kisheria na kijamii (LSAC) na Katibu wa Mara Alliance, Mheshimiwa Ostack Mligo, alisema, mradi huu unaratibiwa na Mara Alliance, kundi la washiriki 13 wanaotekeleza mradi huu ikiwa ni pamoja na; Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika mkoa wa Mara, Graça Machel Trust (GMT), Shirika la Kuelimisha Mtoto: Qatar (EAC), kamati za shule mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali na idara za serikali mkoani Mara. Shirika la kuelimisha Mtoto: Quatar (EAC) wamesaini barua ya kuridhia kuchangia kiasi cha dola la kimarekani milioni mbili ($ milioni mbili) kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Kwa mujibu wa takwimu UNICEF, watoto milioni mbili nchini Tanzania wenye umri kati ya miaka 7 na 13 hawaendi shule. Karibu 60,000 ya watoto hawa wapo katika mkoa wa Mara. Mara Alliance inatarajia kufanya kazi na uongozi wa shule ili kutambua watoto hao.
Mhashamu, Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, kiongozi wa utekelezaji wa mradi huo na mwenyeji wa mradi, Askofu Michael Msonganzila anasema uzinduzi wa mradi Jumanne ni “tukio kubwa”. “Watoto wengi ambao wameacha masomo ni wasichana na ndio waathirika zaidi wa mila na tamaduni, ambazo zinapelekea maumivu na udhalilishaji kwa mtoto wa kike.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa, katika Mkoa wa Mara, mradi huo utakuwa mchakato halisi wa ukombozi wa wasichana kwa vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji katika Jamii. Kwa kuwawezesha wasichana walioacha shule kurudi shule na kupata elimu, mradi huo unatukumbusha umuhimu wa kuwawezesha wanawake kupata elimu kwa maendeleo ya Jamii na Taifa zima.
Ili kuondokana na vikwazo vinavyomzuia mtoto kwenda shule, Mara Alliance imebainisha maeneo ya vipaumbele 12 ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa umakini. Vipaumbele hivyo ni; msaada wa lishe, kukuza afya, maji na usafi wa mazingira, ulinzi na usalama , huduma za ustawi wa jamii, msaada wa kisaikolojia, msaada wa vifaa, mitaala, miundo mizuri ya uongozi, ushiriki wa jamii, miundombinu, maendeleo ya walimu. Vipaumbele 7 kati ya 12 ni huduma muhimu zinazohitajika na watoto kuishi na kustawi, na vingine kuwezesha ufundishaji bora na mazingira ya kufundishia.
Graça Machel Trust inasema mradi huu ni hatua kubwa na mchango katika mapambano dhidi ya ukeketaji na ndoa za utotoni. Utafiti umeonyesha kuwabakiza wasichana shule kuna uwiano wa moja kwa moja katika kupunguza ndoa za utotoni na aina nyingine za ukiukwaji wa haki.
Trust inafanya kazi katika bara la Afrika kwa kutetea haki za wanawake na watoto pamoja na kukuza utawala bora na uongozi. Inatetea haki za watoto kwa njia shirikishi. Pia inatambua kuwa ukosefu wa haki katika eneo moja ni tishio kwa haki nyingine zote, na kwa hiyo tishio kwa ustawi wa jumla wa mtoto.
Njia sahihi za kukuza na Kulinda haki za watoto, Trust inaamini kwamba bila kupoteza mwelekeo wake, isipokuwa haki za watoto zinatolewa kwa kujali, kwa upendo, na kuunga mkono uhusiano wa msingi kati ya familia na Jamii, haki hizi haziwezi kukuza na kulinda ustawi wa mtoto.
Maelezo ya ziada juu ya mradi wa elimu yanapatikana kwenye kielelezo. Maswali, ushauri, maoni na mapendekezo zaidi juu ya mradi huu yaelekezwe:
Graça Machel Trust
Idara ya Mawasiliano
Barua pepe: info@gracamacheltrust.org – tovuti: www.gracamacheltrust.org
AU
Mshiriki wa Mara Alliance Ndugu Ostack Mligo, Mkurugenzi Mtendaji â Asasi ya Msaada wa kisheria na kijamii (LSAC) na Katibu wa Mara Alliance +255 765 143 544 au +255 783 296 310
Barua pepe: wakilimligo@yahoo.com au legal.social@yahoo.com
Tafiti mbalimbali zimefanyika ili kupata idadi ya watoto walioko shule wenye umri kati ya miaka 7 na 13. Kwa mujibu wa tafifi za UNICEF za mwaka 2015 zinaonesha kuwa takribani watoto milioni mbili nchini Tanzania hawapo shuleni, na zaidi ya watoto 60000 wapo katika mkoa wa Mara. Takwimu zinaonesha kuwa kati ya makundi ya watoto wenye miaka kuanzia 7 hadi 13 wanaume ni wengi 1047000 zaidi ya wasichana ambao ni 921000 hawapo shuleni. Pia tafiti nyingine zinaonesha kuwa kama mkoa wa Mara unaweza kubaini wastani wa watoto 13 kati ya shule 803 kila mwaka na kuelezea vikwazo vya elimu, basi lengo la kuwarudisha shule watoto 10000 kila mwaka litawezekana.
Ili kufikia lengo la kuwarudisha 20000 katika shule, washiriki wa Mara Alliance wanaamini kwamba kama uongozi wa shule una uwezo wa kubaini watoto waliopo nje ya shule na kuwa tayari kuwapeleka shule, basi watoto watarudi shule na hakutakuwa na utoro tena. Mpango umejikita kwenya imani kuwa kama serikali, sekta binafsi, asasi zisizo za kiserikali na familia zitaunda umoja ambao utasaidia shule na familia; utapelekea uboreshwaji wa elimu na kupunguza utoro mashuleni.
Historia ya Tanzania
Tanzania bara ina takribani watu milioni 49.2, 51% ni watoto chini ya umri wa miaka 18. Idadi ya watoto katika shule za msingi inakadiriwa kufikia milioni 10.2 ifikapo mwaka 2020. Elimu inaonekana kama sehemu muhimu ya mkakati wa Tanzania kwa ajili ya mageuzi ya kijamii na kiuchumi.
upatikanaji: Tanzania imefanya maendeleo katika upatikanaji wa elimu mwaka 2011/12 katika suala la viwango vya uandikishaji katika ngazi ya shule za awali na msingi. Ripoti ya mwaka 2014 ya Sekta ya Elimu inaonyesha kwamba kulikuwa na upungufu wa viwango vya uandikishaji katika mwaka 2013/14. Viwango vya uandikishaji katika elimu ya awali imepungua kutoka 39.9% mwaka 2012 hadi 35.5% mwaka 2013. Pia uandikishaji wa watoto katika shule za msingi umeonekana kupungua kutoka 92.0% mwaka 2012 hadi 89.7% mwaka 2013.
Usawa: Tanzania imeripoti mafanikio katika usawa wa kijinsia yenye uwiano wa 1: 1 katika shule za msingi zaidi ya malengo ya kimakakati ya milenia. Pamoja na hali hii chanya, kukosekana kwa usawa wa kijinsia na ukosefu wa ajira, hasa katika ongezeko la idadi ya vijana, kuendelea kuwa changamoto.
Takwimu zilizokusanywa na watafiti mbalimbali zinaonesha utofauti. Takwimu za watoto walioko nje ya shule na walioacha pia zinahitajika ili kuelewa na kushughulikia usawa huo.
Ubora: Kumekuwa na kushuka kwa ufaulu katika mitihani na matokeo mabaya ya kujifunza. Mwaka 2012, % 30.7 tu ya wale ambao walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi walifaulu, chini ya 58 .3% ya mwaka 2011. Jamii haihusishwi katika mikakati ya upatikanaji wa elimu bora. Kutokana na tofauti kubwa katika ubora wa elimu kati ya shule na mikoa, wadau, ikiwa ni pamoja na wazazi na jamii, hawana uwezo wa kulinganisha shule zao na za wenzao au taifa kwa ujumla.
Walimu: Kuna ongezeko la idadi ya walimu wa shule za msingi kutoka (180,987 kwa mwaka 2012, hadi 189,487kwa mwaka 2013). Katika kipindi hicho hicho, uwiano wa walimu wenye sifa uliongezeka kutoka 96.6% hadi 99%. Changamoto zaidi ni taarifa katika utoaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na upatikanaji wa miundombinu ya kutosha ya shule. Mazingira duni ya kazi yamepelekea walimu kukata tamaa.
Ongezeko la uandikishaji limepelekea uhaba wa walimu wenye sifa na imepelekea kupungua kwa mbinu mbadala kwa walimu. Walimu wengi kukosa uwezo wa kufundisha masomo inavyotakiwa. Hii ni kweli hasa kwa masomo fulani ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Hisabati na Sayansi . Mafunzo ya jinsia pia yanahitajika kwa walimu ili kuhakikisha mahitaji ya msingi ya wasichana yanashughulikiwa.